UFUNGAJI WA UMEME JUA
KATIKA ZAHANATI 27 WABORESHA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA MASASI
![]() |
Zahanati ya Mbemba iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Masasi inayotumia umeme jua (solar energy) |
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara Mhe Fikiri
Lukanga ameishukuru Halmashauri ya Enzkreis ya nchini ujerumani kwa msaada wao
wa kuweka mifumo ya umeme Jua katika Zahanati 27 na nyumba za watumishi wa afya
51 lengo ikiwa ni kuboresha utoaji wa
huduma za afya kwa wananchi hasa kwa akina mama wajawazito kwa kuwa na umeme wa
uhakika muda.
Lukanga ametoa shukrani
hizo wakati wa tamasha la siku ya umeme jua lililofanyika katika kata ya
Mijelejele wilayani humo liliolenga kuhamasisha wananchi juu ya kuongeza
matumizi ya nishati ambayo ni rafiki wa mazingira na kusema kuwa anaipongeza
wakala ya nishati Jadidifu Tanzania (TAREA)
kwa juhudi wanazozifanya kuhakikisha matumizi ya nishati mbadala hasa
umeme wa jua yanaongezeka.
Aidha Lukanga alifafanua
kuwa nishati ya umeme ni kitu muhimu sana katika ustawi wa jamii kiuchumi na
kijamii kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla hivyo uwepo wa umeme wa wa
uhakika ni uhakika wa maendeleo.
“Kila mtu ni shaidi kadhia kubwa zilizokuwa
zinawapata akina mama wajawazito, watoto, wazee na wagonjwa kwa ujumla kutokana
na kukosekana na nishati mbadala ya umeme katika zahanati zetu, hali hii
inapelekea wauguzi wetu kutumia tochi za simu, vibatali na taa za chemli katika
kutoa huduma nyakati za usiku” alieleza
Satmah.
Nae mwenyekiti wa
Halmashauri ya wilaya ya Masasi mhe Juma
Satmah alieleza kuwa halmashauri za wilaya ya masasi Zinufaika sana na urafiki
huo kwani pamoja na kuweka mifumo ya umeme jua pia wamekuwa wakifanya ziara za
mafunzo kwa viongozi na wanafunzi lengo ikiwa ni kubadilishana mawazo lakini
pia bado kuna mipango ya kufanya biashara pamoja ambapo watunaweza kupeleka
bidhaa za masasi Ujerumani.
“hii ni fursa adhimu sana
kwa wanamasasi tunajivunia ushirikiano huu kati ya Masasi na Enzkreis ya
Ujerumani kwani manufaa yake yananufaisha wananchi kwa ujumla” alisema Satmah
Kwa upande wake
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Changwa Mkwazu amesema
kuwa kupitia mradi huu wa ufungaji wa mifumo ya umeme jua kwenye zahanati 27
hali ya utoaji wa huduma umeimarika sana ambapo wananchi wanapat huduma muda
wote lakini pia wataalamu wa afya wanakaa nyumba ambazo zina umeme hali ambayo
inawafanya wajione wako kwenye mazingira mazingira mazuri ya kufanyia kazi.
Wakiongea kwa niaba ya
wananchi wa masasi, wananchi wa mijelejele wameishukuru serikali kufanya
tamasha hilo la matumizi ya nishati ya umeme jua kwani umeme nihuduma muhimu
katika kufikia maendeleo ikiwemo ya afya , kiuchumi na kijamii kwa ujumla.

Kwa upande wa Mwakilishi
wa wakala ya nishati Jadidifu Tanzania (TAREA)
Emanuela Laswahi alisema kuwa TAREA iko tayari kuhamasisha wananchi kutambua umuhimu wa kutumia umeme Jua
na Nishati nyingine Jadidifu kwa lengo la kulinda mazingira,kuinua uchumi na
kuboresha huduma za jamii kwa ujumla, hivyo “tunasisitiza wananchi waongeze
kazi ya utumiaji wa nishati Jadidifu maana ni rafiki wa mazingira”
Kwa taarifa zaidi tembelea Tovuti yetu ya www.masasidc.go.tz