Friday, 31 March 2017

WANAWAKE WAJENGEWE UWEZO KUELEKEA TANZANIA YA VIWANDA


Mgeni rasmi Bi.Eufrosina Chikojo (Afisa Tawala (W) Masasi akiwahutubia wananchi (hawapo kwenye picha) kwenye maadhimisho ya siku ya  wanawake duniani 2017 yaliyofanyika kiwilaya katika kijiji cha Lukuludi B.


Bi. Eufrosina Chikojo, Afisa Tawala(W) masasi akikagua vikundi vya ujasiriamali kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Lukuledi B siku ya tarehe 08.03.2017


Bi. Eufrosina Chikojo, Afisa Tawala(W) Masasi  akikabidhi hundi za mikopo kwa vikundi vya wajasiliamali vilivyopo kata ya lukuledi  kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Lukuledi B siku ya tarehe 08.03.2017
 Bi. Eufrosina Chikojo, Afisa Tawala(W) Masasi   akiendeea kukabidhi hundi za mikopo kwa vikundi vya wajasiliamali vilivyopo kata ya lukuledi

Thursday, 30 March 2017

MAAFISA HABARI SERIKALI WAMETAKIWA KUTUMIA TOVUTI KUTOA TAARIFA SAHIHI KWA UMMA.
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Evod Mmanda (wa tatu kulia) akizindua moja ya Tovuti iliyotengenezwa siku ya uzinduzi wa tovuti za serikali  zilizotengenezwa kwa udhamini wa Mradi wa uimarishaji wa mifumo ya sekta ya umma (PS3) kwa mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma tarehe 27 machi, 2017 katika ukumbi wa Tiffany Diamond Hotel

 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Evod Mmanda (aliyevaa Tai) akitoa maelezo maafisa Habari na Tehama baada ya kuzindua Tovuti za serikali zilizotengenezwa kwa mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma katika ukumbi wa Tiffany Diamond Hotel machi 27, 2017 (wa kwanza kulia ni kiongozi wa wawezeshaji ndugu Edgar Mdemu


Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara mheshimiwa Evod Mmanda (wa tatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wawezeshaji wa mafuno ya utengenezaji wa Tovuti za serikali
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara mheshimiwa Evod Mmanda (wa tatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya  maafisa Habari na Tehama  waliowezeshwa kutengeneza tovuti za taasisi zao.


Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mheshimiwa Evod Mmanda amewataka  maafisa habari wa taasisi za serikali kuhakikisha wanatumia tovuti za serikali zilizotengenezwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati ili kuepusha changamoto ya upotoshaji taarifa mbalimbali za serikali kwa umma.

Mmanda aliyasema hayo wakati wa kufunga mafunzo ya siku saba ya uanzishaji wa Tovuti za serikali yaliyofanyika katika ukumbi wa Tiffany Diamond Hotel na kueleza kuwa maafisa habari ndio wanawajibu wa kutoa taarifa sahihi kwa umma, hivyo viongozi wa Taasisi za Serikali hawatakiwi kuzuia taarifa muhimu kwa wananchi kuingizwa kwenye Tovuti ili kuimarisha utawala bora unaozingatia uwazi na uwajibikaji kwa umma. 

Mmanda aliongeza kuwa kupitia tovuti hizo wananchi na wadau  wataweza kupata fursa ya kuandika au kutoa malalamiko yao moja kwa moja kwenye tovuti ya taasisi husika na kupata majibu kwa wakati bila kusumbuka kwenda ofisi za Taasisi hiyo hali ambayo itapunguza gharama na upotevu wa muda katika kupata huduma wanayotaka.

“Mnapaswa kufahamu kuwa upatikanaji wa taarifa kwa umma ni suala la kisheria, hivyo uwekaji wa taarifa kwenye tovuti za kutoa taarifa na kutangaza fursa mbalimbali  za uwekezaji zilizopo ni la lazima sio utashi wa mtu ni lazima taarifa hizi zihuishwe kila mara ili ziendane na wakati”  aliagiza Mmanda.

Aidha Mmanda alieleza kuwa Uwekaji wa taarifa za taasisi kwenye tovuti unaweza kuwasaidia  wawekezaji  kujua fursa zilizopo katika taasisizetu kwani atakuwa na uwezo wa kufahamu  awekeze kwenye nini na kwa kiasi gani ili awe kupata faida. 

Kwa Upande wake Mkuu wa timu ya wawezeshaji, Edgar Mdemu amesema mradi huo unaodhaminiwa na USAID umezindukiwa leo kitaifa mjini Dodoma na kwamba wanatarajia matumizi ya Tovuti yatasaidia kuimarisha utawala bora na ushirikishwaji  wa raia katika utekelezaji wa shughuli za serikali kwa uwazi.

Mafunzo ya utengenezaji wa Tovuti yalifunguliwa Machi 20 na kufungwa Machi 27 ambapo kitaifa zoezi la ufungaji limefanyika mjini Dodoma.Uimarishaji wa mifumo ya sekta za umma unaofadhiliwa na shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) ulianza mwaka 2016 na utadumu kwa miaka mitano (5) ambapo jumla ya Halmashauri 93 katika mikoa 13 ya Tanzania bara pamoja na serikali kuu zitanufaika.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara mheshimiwa Evod Mmanda  akiitoa hotua wakati ya kufunga mafunzo ya utengenezaji wa tovuti za serikali  kwa mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma  na  kuzizindua rasmi.

UZINDUZI WA MAFUNZO YA UTENGENEZAJI WA TOVUTI ZA SERIKALI KWA MIKOA YA MTWARA, LINDI NA RUVUMAKatibu tawala wa mkoa wa mtwara ndugu Alfred Luanda akifungua  mafunzo ya utengenezaji wa tovuti za serikali kwa Mikoa  ya Lindi, Mtwara na Ruvuma yaliyofanyika mtwara kuanzia tarehe 20 hadi 27 machi, 2017 
Uimarishaji wa mifumo ya sekta za umma kupitia  mradi wa PS3 ikiwemo uanzishwaji na uhuishwaji wa Tovuti katika taasisi za umma utasaidia  serikali kuimarisha utoaji wa taarifa kwa umma kwa haraka na kwa wakati hali itakayo boresha utawala bora katika kuwahudumia wananchi kwa uwazi.

Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara ndugu Alfred Luanda wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya utengenezaji wa tovuti za serikali kwa mikoa  ya Lindi, Mtwara na Ruvuma yaliyofanyika kwa muda wa siku nane kuanzia tarehe 20 hadi 27, Machi, 2017 na kueleza kuwa mafunzo hayo yatawajengea uwezo Maafisa Habari na TEHAMA kuweza kuendesha tovuti za serikali vizuri katika kuwahabarisha wananchi. 

Luanda amewaeleza washiriki kuwa uboreshaji wa tovuti za serikali utawezesha wananchi kupata fursa na haki ya kupata habari na taarifa kwa njia ya mtandao  ambayo ndio njia ya haraka zaidi.

“Mnapaswa kufahamu kuwa upatikanaji wa taarifa kwa umma ni suala la kisheria, hivyo baada ya mafunzo haya mtakuwa mmepata uwezo zaidi wa kuandaa na kutangaza taarifa na fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo kwenye taasisi zenu”  alifafanua Luanda 

Uimarishaji wa mifumo ya sekta za umma unaofadhiliwa na shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) ulianza mwaka 2016 na utadumu kwa miaka mitano (5) ambapo jumla ya Halmashauri 93 katika mikoa 13 ya Tanzania bara pamoja na serikali kuu zitanufaika.