Tuesday 12 February 2019

BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI LAPITISHA BAJETI YA SHILINGI BIL 34.4 KWA MWAKA 2019/2020


 Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mhe LEODGER Chilala (wa kwanza  kushoto) wakati akifungua mkutano wa baraza la Madiwani  la  kujadili na kupitisha Rasimu ya Bajeti kwa mwaka 2019/2020 ( wa katikakti ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Bi Changwa Mkwazu)


Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ndugu Jelemiah Lubeleje akiwasilisha Rasimu ya Bajeti kwa kwa mwaka 2019/2020 
 kwenye  mkutano wa baraza la Madiwani  la  kujadili na kupitisha Rasimu ya Bajeti leo tarehe 12.02.2019
Waheshimiwa madiwani wakiwa kwenye mkutano wa baraza la Madiwani  la  kujadili na kupitisha Rasimu ya Bajeti leo tarehe 12.02.2019

 Waheshimiwa madiwani wakiwa kwenye mkutano wa baraza la Madiwani  la  kujadili na kupitisha Rasimu ya Bajeti leo tarehe 12.02.2019


Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara imejadilili  imepitisha mapendekezo ya rasimu ya mpango  wa bajeti  zaidi ya shilingi bilioni  34.4 kwa   mwaka 2019/2020  kwa ajili ya matumizi ya kawaida na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. 
 
Mapendekezo hayo yamepitishwa leo na Baraza la Madiwani katika Mkutano  maalum wa kupitisha rasimu hiyo uliofanyika katika  ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.

Akiwasilisha mapendekezo ya rasimu ya  bajeti hiyo katika baraza la madiwani, Afisa Mipango wa Halmashauri ndugu Jeremiah Lubeleje  kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Chwangwa Mkwazu, alisema kuwa   lengo la Halmashauri ni kukusanya  shilingi bilioni 34.4 ambapo kati za hizo zaidi ya shilingi bilioni 2.3 ni mapato ya ndani.

Kwa mapato ya ndani, Halmashauri itakusanya kupitia ushuru wa mazao kilimo, ushuru wa mazao ya misitu, ushuru wa huduma,  madini ya ujenzi, leseni za biashara, ada za upimaji mashamba, stendi na vyanzo vingine

Lubeleje alifafanua kuwa  kwenye matumizi mengineyo Halmashauri imepanga kutumia shilingi bilioni 1.02,  kwa ajili ya miradi ya maendeleo jumla ya shilingi bilioni 4.3  kwa upande wa mishahara zaidi ya bilioni 26.7 zimepangwa kutumika kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Juma Satmah  alisema  kuwa kwa bajeti hiyo Halmashauri imeongeza vyanzo vya mapato ili kuoboresha utendaji kazi wa kuhudumia wananchi ikiwemo utekelezaji wa miradi ampao katika mwaka 2019/2020 hamashauri itatumia zaidi ya bilioni 1.1 kutoka atika mapato ya ndani kwa ajili ya kutekelezaji wa miradi ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya shule.

Satmah aliongeza kuwa  bajeti hiyo pia imelenga kuimarisha kuimarisha sekta ya kilimo mifugo na uvuvi ili kuboresha sekta hio ukizingatia  sehemu kuwa ya mapato ya ndani ya halmashauri hiyo  yanatokana na kilimo ambapo shilingi milioni 181,532,000 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa ghala la mazao pamoja na kuanzisha shamba darasa.

Aidha mwenyekiti amesema bajeti hiyo imezingatia kutoa mchango wa asilimia kumi (10%)  wananwake na vijana kutoka mapato ya ndani.

No comments:

Post a Comment