Friday 31 March 2017

WANAWAKE WAJENGEWE UWEZO KUELEKEA TANZANIA YA VIWANDA


Mgeni rasmi Bi.Eufrosina Chikojo (Afisa Tawala (W) Masasi akiwahutubia wananchi (hawapo kwenye picha) kwenye maadhimisho ya siku ya  wanawake duniani 2017 yaliyofanyika kiwilaya katika kijiji cha Lukuludi B.


Bi. Eufrosina Chikojo, Afisa Tawala(W) masasi akikagua vikundi vya ujasiriamali kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Lukuledi B siku ya tarehe 08.03.2017


Bi. Eufrosina Chikojo, Afisa Tawala(W) Masasi  akikabidhi hundi za mikopo kwa vikundi vya wajasiliamali vilivyopo kata ya lukuledi  kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Lukuledi B siku ya tarehe 08.03.2017
 Bi. Eufrosina Chikojo, Afisa Tawala(W) Masasi   akiendeea kukabidhi hundi za mikopo kwa vikundi vya wajasiliamali vilivyopo kata ya lukuledi


Katika kuelekea Tanzania ya viwanda, ili wananwake wawe msingi wa mabadiliko kiuchumi inapaswa wajengewe uwezo wa kitaaluma, kibiashara, upatikanaji wa masoko na mikopo ili waweze kushiriki kwa usawa na kunufaika na fursa zilizopo badala ya kuwa wasindikizaj.

Hayo yalisemwa na mwakilisha wa Mkuu wa Wilaya ya Masasi Bi. Eufrosina Chikojo wakati akiwahutubia wananchi katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kiwilaya katika Kata ya Lukuledi wilayani Masasi na kusisitiza kuwa ili wananwake waweze kushiriki kwenye uchumi wa viwanda ni lazima wapewe elimu ya kutambua fursa zilizopo na namna ya kuzitumia.

Chikojo alisema kuwa kauli  mbiu ya siku hii ya wananwake inayosema Tanzania ya viwanda, wanawake ni msingi wa mabadiliko ya kiuchumi ”, itatekelezwa kwa vitendo endapo mwananke atapata elimu ya kutosha itakayo mwezesha  kutambua na kutumia fura za kibiashara katika kukuza uchumi wa kaya na taifa kwa ujumla kwani wao ndio walezi wakuu wa familia katik jamii zetu.

Hivyo, kutokana na mabadiliko tunayoyaendea kuna haja ya wanaume na jamii kwa ujumla  kuona umhimu wa kumkinga  mtoto wa kike  na madhara mabaya ikiwemo kutompeleka shule, ndoa za utotoni na tatizo la mimba kwa kuwa ndiye mwenye nafasi kubwa katika kulea familia na jamii kwa ujumla.

Katika kuwawezesha wanawake Halmashauri inapaswa kutenga fedha asilimia tano (5%) ya mapato yake ndani ili kuweza kuwakopesha kwa riba nafuu. Aliwatia moyo akina mama waliokopeshwa fedha na Halmashauri kufanya marejesho kwa ufasaha ili wengine waweze kupata mikopo hiyo.

Bi. Chikojo amekemea tabia ya wanaume kuwabagua wanawake kwa kuwanyima haki yao ya msingi ya kumiliki raslimali zikiwemo ardhi, nyumba, mifugo na fursa zingine za kiuchumi pamoja na kutowashirikisha  katika utoaji wa maamuzi ndani ya familia iachwe kwani  nchi yetu inapoelekea katika uchumi wa viwanda wanaume wanapaswa kutoa fursa kwa wanawake kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali.

Katika maadhimisho hayo Bi Chikojo alikabidhi hundi za jumla ya shilingi 125,500,000/= kwa vikundi 72 kati ya fedha hizo shilingi 54,900,000/= zilizokabidhiwa kwa vikundi 27 vya wanawake na jumla ya wanawake 587 watanufaika na mikopo hiyo.



 wanavikundi  wakionesha bidhaa mbele ya mgeni rasmi

 




No comments:

Post a Comment