Tuesday 18 December 2018

JAMII YASISITIZWA MATUMIZI YA NISHATI MBADALA


UFUNGAJI WA  UMEME JUA KATIKA ZAHANATI 27 WABORESHA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA MASASI

Zahanati ya Mbemba iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Masasi  inayotumia umeme jua (solar energy)

Mwakilishi wa Mkuu wa  Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara Mhe Fikiri Lukanga ameishukuru Halmashauri ya Enzkreis ya nchini ujerumani kwa msaada wao wa kuweka mifumo ya umeme Jua katika Zahanati 27 na nyumba za watumishi wa afya 51 lengo ikiwa ni kuboresha  utoaji wa huduma za afya kwa wananchi hasa kwa akina mama wajawazito kwa kuwa na umeme wa uhakika muda. 

Lukanga ametoa shukrani hizo wakati wa tamasha la siku ya umeme jua lililofanyika katika kata ya Mijelejele wilayani humo liliolenga kuhamasisha wananchi juu ya kuongeza matumizi ya nishati ambayo ni rafiki wa mazingira na kusema kuwa anaipongeza wakala ya nishati Jadidifu Tanzania (TAREA)  kwa juhudi wanazozifanya kuhakikisha matumizi ya nishati mbadala hasa umeme wa jua yanaongezeka.

Aidha Lukanga alifafanua kuwa nishati ya umeme ni kitu muhimu sana katika ustawi wa jamii kiuchumi na kijamii kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla hivyo uwepo wa umeme wa wa uhakika ni uhakika wa maendeleo.

 “Kila mtu ni shaidi kadhia kubwa zilizokuwa zinawapata akina mama wajawazito, watoto, wazee na wagonjwa kwa ujumla kutokana na kukosekana na nishati mbadala ya umeme katika zahanati zetu, hali hii inapelekea wauguzi wetu kutumia tochi za simu, vibatali na taa za chemli katika kutoa huduma nyakati za usiku”  alieleza Satmah.

Nae mwenyekiti wa Halmashauri  ya wilaya ya Masasi mhe Juma Satmah alieleza kuwa halmashauri za wilaya ya masasi Zinufaika sana na urafiki huo kwani pamoja na kuweka mifumo ya umeme jua pia wamekuwa wakifanya ziara za mafunzo kwa viongozi na wanafunzi lengo ikiwa ni kubadilishana mawazo lakini pia bado kuna mipango ya kufanya biashara pamoja ambapo watunaweza kupeleka bidhaa za masasi Ujerumani.

“hii ni fursa adhimu sana kwa wanamasasi tunajivunia ushirikiano huu kati ya Masasi na Enzkreis ya Ujerumani kwani manufaa yake yananufaisha wananchi kwa ujumla” alisema Satmah

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Changwa Mkwazu amesema kuwa kupitia mradi huu wa ufungaji wa mifumo ya umeme jua kwenye zahanati 27 hali ya utoaji wa huduma umeimarika sana ambapo wananchi wanapat huduma muda wote lakini pia wataalamu wa afya wanakaa nyumba ambazo zina umeme hali ambayo inawafanya wajione wako kwenye mazingira mazingira mazuri ya kufanyia kazi.


Wakiongea kwa niaba ya wananchi wa masasi, wananchi wa mijelejele wameishukuru serikali kufanya tamasha hilo la matumizi ya nishati ya umeme jua kwani umeme nihuduma muhimu katika kufikia maendeleo ikiwemo ya afya , kiuchumi na kijamii kwa ujumla.
 


Kwa upande wa Mwakilishi wa wakala ya nishati Jadidifu Tanzania (TAREA)  Emanuela Laswahi alisema kuwa TAREA iko tayari kuhamasisha  wananchi kutambua umuhimu wa kutumia umeme Jua na Nishati nyingine Jadidifu kwa lengo la kulinda mazingira,kuinua uchumi na kuboresha huduma za jamii kwa ujumla, hivyo “tunasisitiza wananchi waongeze kazi ya utumiaji wa nishati Jadidifu maana ni rafiki wa mazingira” 

Kwa taarifa zaidi tembelea Tovuti yetu ya www.masasidc.go.tz