Saturday 9 March 2019

WANAWAKE WATAKIWA KUWA NA MATAZAM CHANYA KUFIKIA USAWA WA KIJINSIA




Mgeni rasmi  Bi Emmy Rajab Ng’oura akuhutubia wananchi wa Mchauru siku ya maadhimisho ya Wananwake Dudiani Halmashauri ya wilaya ya masasi
 
Ili kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya Maadhimisho ya siku ya wanawake kwa mwaka 2019 isemayo “Badili fikra, kufikia usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu” Wanawake wametakiwa kuwa na mtazamo chanya kufikia maendeleo  katika Nyanja mbalimbali ikiwemo kiuchumi, kisiasa, kijamii pamoja na  kuwa mfano bora kwa malezi ya watoto ili kuwa na jamii yenye maadili mema.



Kauli hiyo ilitolewa na Mgeni rasmi  Bi Emmy Rajab Ng’oura  ambaye ni Afisa  Tarafa  wa tarafa ya Lulindi , Halmashauri ya Wilaya ya masasi , katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wanawake duniani , yaliyofanyika jana machi , 8 katika  viwanja vya shule ya sekondari Namombwe kata ya Mchaulu.

Akihutubia wananchi wakati wa sherehe hizo, Bi Ng’oura  amewataka wanawake wa halmashauri hiyo, kubadili fikra hasi katika kufikia maendeleo, badala yake  watumie fursa zinazotolewa na serikali na wadau mbalimbali ikiwemo utoaji wa mikopo isiyo na riba,  elimu ya masuala ya usawa wa kijinsia  na vitambulisho vya wajasiliamali  ili kujikwamua wenyewe katika sekta zote  na kutekeleza majukumu yao bila vikwazo vinavyotokana na jinsia.
Mgeni rasmi  Bi Emmy Rajab Ng’oura akishiri zoezi la ufyatuaji wa tofali kwa ajili a ujenzi wa Bweni la  wasichana katika shule ya sekondari Nambombwe
 
Bi Ng’oura  alieleza kuwa  “Moja ya fursa ambayo serikali imeitoa ni kutoa vitambulisho vya wajasiliamali wadogo kwa bei ya shiringi 20,000 tu, nawasihi wanawake wanaojihusisha na ujasiliamali kuchangamukia fursa hii ili muweze kufanya biashara zenu bila usumbufu wa kutoa tozo zingine zozote”

Mgeni rasmi  Bi Emmy Rajab Ng’oura akimvalisha kitambulisho cha ujasiliamali mmoja ya wanawake katika siku ya maadhimisho ya  wanawake duniani


Aidha  alisema kuwa , kumekuwa na matukio mbalimbali ya ukatili kwa watoto, wananwake inawapasa kuwa mstari wa mbele kupinga na kuwafichua watu wanaofanya ukatili wa kijinsia na wale waliofanyiwa ukatili kama ubakaji na ndoa za utotoni, ili kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto na sio kuungana nao kuwaficha wahalifu hao.

" Ni vema kutambua, wanawake ndio msingi wa mabadiliko kwenye jamii, kama wanawake tutabadili fikra zetu juu ya mambo mbalimbali  kuanzia ndani ya familia, jamii zetu  pia zitabadika, hakutakuwa na ukatili na udhalilishaji kwa wanawake na watoto, watoto wote watapata elimu sawa bila kujali jinsia na tutatokomeza ndoa na mimba za utotoni.

Ni jambo la kujivunia kuona Kadri ya siku zinavyoenda wanawake wanashika nyazifa tofauti katika sekta mbalimbali kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa, ambapo kwa Halmashauri hiyo jumla ya wananwake 104 wanatumikia nafasi mbalimbali za uongozi “ haya ni mafanikio makubwa tunapaswa kujipongeza” alieleza Bi Ng’oura 

Akisoma  taarifa ya utekelezaji  mbele ya mgeni rasmi, Afisa Maendeleo ya Jamii na Jinsia, Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Neema Joseph amesema kuwa, Halmashauri hiyo imefanya maadhimisho hayo, huku ikiwa na mafanikio makubwa katika kuwawezesha wanawake  na vijana kiuchumi,  ambapo jumla vikundi 8,vimepatiwa mikopo ya bila riba, yenye thamani ya shilingi milioni 75, fedha zinazotokana na asilimia 10 za mapato ya ndani kwa mwaka huu wa fedha 2018/2019.
Afisa Maendeleo ya Jamii na Jinsia, Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Neema Joseph akisoma taarifa ya utekelezaji
 
Pamoja na kuadhimisha maadhimisho yaho kihalmashauri katika kata ya mchaulu, afisa maendeleo ya jamii alieleza kuwa sherehe kama hizo pia zinafanywa katika kata zingine kama Mwena, ndanda, chigugu na Nangoo, lengo ikiwa ni kuhasisha wanawake katika maeneo yote kutambua haki na wajibu katika kufikia usawa wa kijinsia ambapo wameshiriki katika shunguli mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa miradi, kufanya usafi , kusaidia wagonjwa na kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu
Mgeni rasmi  Bi Emmy Rajab Ng’oura akikabidhi vifaa vya shule kwa wanafunzi waishio katika mazingira magumu vilivyotolewa na Chama cha walimu (CWT)
 
Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ya "Badili Fikra Kufikia Usawa wa Kijinsia kwa Maendeleo Endelevu" yamekwenda sambamba na upimaji wa afya kwa magonjwa yanayoambukizwa na yasiyoambukizwa bure, burudani mbalimbali, mashindano ya mchezo wa mpira wa miguu kwa wananwake na  mpira wa pete.
  

Wednesday 6 March 2019

WATENDAJI KATA,VIJIJI NA MITAA MASASI WAPIGWA MSASA KODI YA MAJENGO




Katibu Tawala wa Wilaya ya Masasi Azizi Fakiri (aliyesimama) akifungua kikao cha TRA na watendaji wa kata, vijiji na Mitaa Wilaya ya Masasi jana tarehe 05.03.2019 katika ukumbi wa Nursing Mkomaindo kuhusu kodi ya Majengo.



 Mamlaka ya Mpato Tanzania (TRA)  Wilayani masasi, imewaomba watendaji wa kata, vijiji na mitaa katika Halmashauri ya wilaya na mji Masasi kusaidia ukusanyaji wa kodi ya majengo katika maeneo yao ili kufanikisha ukusanyaji wa mapato ya serikali kupitia chanzo hicho.


Akizungumza katika kikao cha TRA na watendaji hao, Afisa mapato wa TRA Mkoa wa Mtwara  Edwin Nkinga alisema,  kodi ya majengo inatozwa kwa nyumba zilizopo katika maeneo yote yaani kuanzia ngazi ya vijiji, mitaa na kata ndio maana watendaji wanahusika moja kwa moja kutambua nyumba zote zilizopo katika maeneo yao ili zilipiwe kodi kama sheria inavyoelekeza .
  Afisa mapato wa TRA Mkoa wa Mtwara  Edwin Nkinga akitoa maelekezo kwa watendaji

Nkinga  alieleza kuwa “Kikao hiki kinalenga kuwaelimisha  nyinyi watendaji  ili muweze kujua  wajibu na majuku yenu  katika ukusanyaji wa kodi za majengo ambapo majengo yanayotozwa kodi ni yale yanayotumika” 

Nkinga alifafanua kuwa, Sheria ya kodi ya majengo inataja kiasi cha kodi kuwa ni shilingi 10,000 kwa nyumba za kawaida 20,000 kwa majengo ya ghorofa maeneo ya vijijini na 50,000 kwa majengo ya ghorofa maeneo ya mijini.  

Aidha Nkinga alieleza kuwa baadhi ya majengo yanapata msamaha wa kodi yakiwemo majengo yanayotumiwa na Taasisi za Umma, majumba ya makumbusho au maktaba, majengo ndani ya makaburi, nyuma zilizoezekwa kwa nyasi na  za udongo

 Watendaji wa kata, vijiji na mitaa wakiwa kwenye kikao
 
Alisema watendaji hao wanatakiwa kusimamia ukusanyaji wa kodi za majengo katika maeneo yao kwa kutumia mfumo wa bili za majengo kutoka TRA kwa kutambua nyumba zote zilizopo kwenye maeneo yao kwa kujaza fomu kila mwaka ili kutambua idadi ya nyuma zilizopo  na hatimaye ziweze kuliiwa kodi kulingana na hadhi ya jengo husika.

Kodi za majengo ni chanzo kingine cha mapato ya serikali, hivyo watendaji wote wanatakiwa  kwa ajili ya nyumba zote zinazostahili kulipa kodi kwenye daftari la makazi katika maeneo yao.

Watendaji wa kata, vijiji na mitaa wakifurahia jambo  kwenye kikao


 Alisema sheria ya utoaji kodi ya majengo ya mwaka 1983 imeainisha maeneo yanayotozwa kodi ya majengo kuwa ni Halmashauri za miji, majiji, manspaa na wilaya.

Awali kodi za majengo ilikuwa inakusanywa na Halmashauri zote nchini, lakini mwaka 2016 kupitia bunge la bajeti serikali ilirekebisha sheria kodi ya majengo na kuipa TRA jukumu la kukadilia,kukusanya na kuhesabu kodi ya majengo katika halmashauri zote nchini.
 
Aidha, alisema  kuwa kwa atakae kaidi kulipa kodi  kwa wakti  atachukuliwa hatua ikiwemo  kulipa  riba  kama adhabu, kufikishwa mahakamani  au kukamatiwa mali zake na kuuzwa ili kulipa kodi anayodaiwa.

Tuesday 12 February 2019

BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI LAPITISHA BAJETI YA SHILINGI BIL 34.4 KWA MWAKA 2019/2020


 Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mhe LEODGER Chilala (wa kwanza  kushoto) wakati akifungua mkutano wa baraza la Madiwani  la  kujadili na kupitisha Rasimu ya Bajeti kwa mwaka 2019/2020 ( wa katikakti ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Bi Changwa Mkwazu)


Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ndugu Jelemiah Lubeleje akiwasilisha Rasimu ya Bajeti kwa kwa mwaka 2019/2020 
 kwenye  mkutano wa baraza la Madiwani  la  kujadili na kupitisha Rasimu ya Bajeti leo tarehe 12.02.2019
Waheshimiwa madiwani wakiwa kwenye mkutano wa baraza la Madiwani  la  kujadili na kupitisha Rasimu ya Bajeti leo tarehe 12.02.2019

 Waheshimiwa madiwani wakiwa kwenye mkutano wa baraza la Madiwani  la  kujadili na kupitisha Rasimu ya Bajeti leo tarehe 12.02.2019

Tuesday 18 December 2018

JAMII YASISITIZWA MATUMIZI YA NISHATI MBADALA


UFUNGAJI WA  UMEME JUA KATIKA ZAHANATI 27 WABORESHA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA MASASI

Zahanati ya Mbemba iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Masasi  inayotumia umeme jua (solar energy)

Mwakilishi wa Mkuu wa  Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara Mhe Fikiri Lukanga ameishukuru Halmashauri ya Enzkreis ya nchini ujerumani kwa msaada wao wa kuweka mifumo ya umeme Jua katika Zahanati 27 na nyumba za watumishi wa afya 51 lengo ikiwa ni kuboresha  utoaji wa huduma za afya kwa wananchi hasa kwa akina mama wajawazito kwa kuwa na umeme wa uhakika muda. 

Lukanga ametoa shukrani hizo wakati wa tamasha la siku ya umeme jua lililofanyika katika kata ya Mijelejele wilayani humo liliolenga kuhamasisha wananchi juu ya kuongeza matumizi ya nishati ambayo ni rafiki wa mazingira na kusema kuwa anaipongeza wakala ya nishati Jadidifu Tanzania (TAREA)  kwa juhudi wanazozifanya kuhakikisha matumizi ya nishati mbadala hasa umeme wa jua yanaongezeka.

Aidha Lukanga alifafanua kuwa nishati ya umeme ni kitu muhimu sana katika ustawi wa jamii kiuchumi na kijamii kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla hivyo uwepo wa umeme wa wa uhakika ni uhakika wa maendeleo.

 “Kila mtu ni shaidi kadhia kubwa zilizokuwa zinawapata akina mama wajawazito, watoto, wazee na wagonjwa kwa ujumla kutokana na kukosekana na nishati mbadala ya umeme katika zahanati zetu, hali hii inapelekea wauguzi wetu kutumia tochi za simu, vibatali na taa za chemli katika kutoa huduma nyakati za usiku”  alieleza Satmah.

Nae mwenyekiti wa Halmashauri  ya wilaya ya Masasi mhe Juma Satmah alieleza kuwa halmashauri za wilaya ya masasi Zinufaika sana na urafiki huo kwani pamoja na kuweka mifumo ya umeme jua pia wamekuwa wakifanya ziara za mafunzo kwa viongozi na wanafunzi lengo ikiwa ni kubadilishana mawazo lakini pia bado kuna mipango ya kufanya biashara pamoja ambapo watunaweza kupeleka bidhaa za masasi Ujerumani.

“hii ni fursa adhimu sana kwa wanamasasi tunajivunia ushirikiano huu kati ya Masasi na Enzkreis ya Ujerumani kwani manufaa yake yananufaisha wananchi kwa ujumla” alisema Satmah

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Changwa Mkwazu amesema kuwa kupitia mradi huu wa ufungaji wa mifumo ya umeme jua kwenye zahanati 27 hali ya utoaji wa huduma umeimarika sana ambapo wananchi wanapat huduma muda wote lakini pia wataalamu wa afya wanakaa nyumba ambazo zina umeme hali ambayo inawafanya wajione wako kwenye mazingira mazingira mazuri ya kufanyia kazi.


Wakiongea kwa niaba ya wananchi wa masasi, wananchi wa mijelejele wameishukuru serikali kufanya tamasha hilo la matumizi ya nishati ya umeme jua kwani umeme nihuduma muhimu katika kufikia maendeleo ikiwemo ya afya , kiuchumi na kijamii kwa ujumla.
 


Kwa upande wa Mwakilishi wa wakala ya nishati Jadidifu Tanzania (TAREA)  Emanuela Laswahi alisema kuwa TAREA iko tayari kuhamasisha  wananchi kutambua umuhimu wa kutumia umeme Jua na Nishati nyingine Jadidifu kwa lengo la kulinda mazingira,kuinua uchumi na kuboresha huduma za jamii kwa ujumla, hivyo “tunasisitiza wananchi waongeze kazi ya utumiaji wa nishati Jadidifu maana ni rafiki wa mazingira” 

Kwa taarifa zaidi tembelea Tovuti yetu ya www.masasidc.go.tz 

Monday 22 May 2017

MATUKIO KATIKA PICHA MWENGE WA UHURU 2017 HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI TAREHE 14.05.2017

 Mwenge wa Uhuru ukiwa kwenye eneo la makabidhiano katika kijiji cha Nanyindwa kata ya Chiwale tayari kwa kuanza kukimbizwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi.
 Kati Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi wakiushangilia mwenge eneo la mapokezi
  Waheshimiwa madiwani wengine wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi  wakiushangilia mwenge eneo la mapokezi
 Mwanakikundi akitoa maelezo mbele ya mkimbiza mwenge kitaifa ndugu Bahati Lugodisha eneo la lukuledi kabla ya kukabidhiwa hundi za mikopo.
 Wakimbiza mwenge kitaifa wakiwa katika picha ya pamoja na wananfunzi wa shule maalumu ya lukuledi wenye ulemavu wa kutokusikia

 Viongozi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Masasi mhe. Selemani Mzee wakiwa kwenye eneo la kukabidhi mwenge wa uhuru wilaya ya Newala baada ya kumaliza kuukimbza katika Wilaya ya Masasi.


Watu wakicheza wakiwa wanasubilri kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru