Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mhe LEODGER Chilala (wa kwanza kushoto) wakati akifungua mkutano wa baraza la Madiwani la kujadili na kupitisha Rasimu ya Bajeti kwa mwaka 2019/2020 ( wa katikakti ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Bi Changwa Mkwazu)
Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ndugu Jelemiah Lubeleje akiwasilisha Rasimu ya Bajeti kwa kwa mwaka 2019/2020
kwenye mkutano wa baraza la Madiwani la kujadili na kupitisha Rasimu ya Bajeti leo tarehe 12.02.2019
Waheshimiwa madiwani wakiwa kwenye mkutano wa baraza la Madiwani la kujadili na kupitisha Rasimu ya Bajeti leo tarehe 12.02.2019
Waheshimiwa madiwani wakiwa kwenye mkutano wa baraza la Madiwani la kujadili na kupitisha Rasimu ya Bajeti leo tarehe 12.02.2019
Halmashauri
ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara imejadilili imepitisha mapendekezo ya rasimu ya mpango wa
bajeti zaidi ya shilingi bilioni 34.4 kwa
mwaka 2019/2020 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo.
Mapendekezo
hayo yamepitishwa leo na Baraza la Madiwani katika Mkutano maalum wa kupitisha rasimu hiyo uliofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri
hiyo.
Akiwasilisha
mapendekezo ya rasimu ya bajeti
hiyo katika baraza la madiwani, Afisa Mipango wa Halmashauri ndugu Jeremiah
Lubeleje kwa niaba ya Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri hiyo Chwangwa Mkwazu, alisema kuwa lengo
la Halmashauri ni kukusanya shilingi
bilioni 34.4 ambapo kati za hizo zaidi ya shilingi bilioni 2.3 ni mapato ya
ndani.
Kwa
mapato ya ndani, Halmashauri itakusanya kupitia ushuru wa mazao kilimo, ushuru
wa mazao ya misitu, ushuru wa huduma,
madini ya ujenzi, leseni za biashara, ada za upimaji mashamba, stendi na
vyanzo vingine
Lubeleje
alifafanua kuwa kwenye matumizi
mengineyo Halmashauri imepanga kutumia shilingi bilioni 1.02, kwa ajili ya miradi ya maendeleo jumla ya
shilingi bilioni 4.3 kwa upande wa
mishahara zaidi ya bilioni 26.7 zimepangwa kutumika kwa mwaka wa fedha
2019/2020.
Kwa
upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Juma Satmah alisema kuwa kwa bajeti hiyo Halmashauri imeongeza
vyanzo vya mapato ili kuoboresha utendaji kazi wa kuhudumia wananchi ikiwemo
utekelezaji wa miradi ampao katika mwaka 2019/2020 hamashauri itatumia zaidi ya
bilioni 1.1 kutoka atika mapato ya ndani kwa ajili ya kutekelezaji wa miradi
ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya shule.
Satmah
aliongeza kuwa bajeti hiyo pia imelenga
kuimarisha kuimarisha sekta ya kilimo mifugo na uvuvi ili kuboresha sekta hio
ukizingatia sehemu kuwa ya mapato ya
ndani ya halmashauri hiyo yanatokana na
kilimo ambapo shilingi milioni 181,532,000 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa
ghala la mazao pamoja na kuanzisha shamba darasa.
Aidha mwenyekiti amesema bajeti hiyo imezingatia
kutoa mchango wa asilimia kumi (10%) wananwake na vijana kutoka mapato ya ndani.
No comments:
Post a Comment