Mgeni rasmi Bi Emmy Rajab Ng’oura akuhutubia wananchi wa Mchauru siku ya maadhimisho ya Wananwake Dudiani Halmashauri ya wilaya ya masasi
Ili kutekeleza kwa
vitendo kauli mbiu ya Maadhimisho ya siku ya wanawake kwa mwaka 2019 isemayo “Badili
fikra, kufikia usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu” Wanawake wametakiwa kuwa
na mtazamo chanya kufikia maendeleo
katika Nyanja mbalimbali ikiwemo kiuchumi, kisiasa, kijamii pamoja na kuwa mfano bora kwa malezi ya watoto ili kuwa
na jamii yenye maadili mema.
Kauli hiyo ilitolewa na Mgeni
rasmi Bi Emmy Rajab Ng’oura ambaye
ni Afisa Tarafa wa tarafa ya Lulindi , Halmashauri ya Wilaya
ya masasi , katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wanawake duniani , yaliyofanyika
jana machi , 8 katika viwanja vya shule
ya sekondari Namombwe kata ya Mchaulu.
Akihutubia wananchi
wakati wa sherehe hizo, Bi Ng’oura amewataka wanawake wa halmashauri hiyo,
kubadili fikra hasi katika kufikia maendeleo, badala yake watumie fursa zinazotolewa na serikali na
wadau mbalimbali ikiwemo utoaji wa mikopo isiyo na riba, elimu ya masuala ya usawa wa kijinsia na vitambulisho vya wajasiliamali ili kujikwamua wenyewe katika sekta zote na kutekeleza majukumu yao bila vikwazo
vinavyotokana na jinsia.
Mgeni rasmi Bi Emmy Rajab Ng’oura akishiri zoezi la ufyatuaji
wa tofali kwa ajili a ujenzi wa Bweni la wasichana katika shule ya
sekondari Nambombwe
Bi Ng’oura alieleza
kuwa “Moja ya fursa ambayo serikali
imeitoa ni kutoa vitambulisho vya wajasiliamali wadogo kwa bei ya shiringi
20,000 tu, nawasihi wanawake wanaojihusisha na ujasiliamali kuchangamukia fursa
hii ili muweze kufanya biashara zenu bila usumbufu wa kutoa tozo zingine zozote”
Mgeni rasmi Bi Emmy Rajab Ng’oura akimvalisha kitambulisho cha ujasiliamali mmoja ya wanawake katika siku ya maadhimisho ya wanawake duniani
Aidha alisema kuwa , kumekuwa na
matukio mbalimbali ya ukatili kwa watoto, wananwake inawapasa kuwa mstari wa
mbele kupinga na kuwafichua watu wanaofanya ukatili wa kijinsia na wale
waliofanyiwa ukatili kama ubakaji na ndoa za utotoni, ili kutokomeza ukatili
dhidi ya wanawake na watoto na sio kuungana nao kuwaficha wahalifu hao.
" Ni vema kutambua,
wanawake ndio msingi wa mabadiliko kwenye jamii, kama wanawake tutabadili fikra
zetu juu ya mambo mbalimbali kuanzia
ndani ya familia, jamii zetu pia zitabadika,
hakutakuwa na ukatili na udhalilishaji kwa wanawake na watoto, watoto wote
watapata elimu sawa bila kujali jinsia na tutatokomeza ndoa na mimba za
utotoni.
Ni jambo la kujivunia
kuona Kadri ya siku zinavyoenda wanawake wanashika nyazifa tofauti katika sekta
mbalimbali kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa, ambapo kwa Halmashauri hiyo
jumla ya wananwake 104 wanatumikia nafasi mbalimbali za uongozi “ haya
ni mafanikio makubwa tunapaswa kujipongeza” alieleza Bi Ng’oura
Akisoma taarifa ya utekelezaji mbele ya mgeni rasmi, Afisa Maendeleo ya Jamii
na Jinsia, Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Neema Joseph amesema kuwa, Halmashauri
hiyo imefanya maadhimisho hayo, huku ikiwa na mafanikio makubwa katika
kuwawezesha wanawake na vijana kiuchumi,
ambapo jumla vikundi 8,vimepatiwa mikopo
ya bila riba, yenye thamani ya shilingi milioni 75, fedha zinazotokana na
asilimia 10 za mapato ya ndani kwa mwaka huu wa fedha 2018/2019.
Afisa Maendeleo ya Jamii na Jinsia, Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Neema Joseph akisoma taarifa ya utekelezaji
Pamoja na kuadhimisha
maadhimisho yaho kihalmashauri katika kata ya mchaulu, afisa maendeleo ya jamii
alieleza kuwa sherehe kama hizo pia zinafanywa katika kata zingine kama Mwena,
ndanda, chigugu na Nangoo, lengo ikiwa ni kuhasisha wanawake katika maeneo yote
kutambua haki na wajibu katika kufikia usawa wa kijinsia ambapo wameshiriki
katika shunguli mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa miradi, kufanya usafi
, kusaidia wagonjwa na kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu
Mgeni rasmi Bi Emmy Rajab Ng’oura akikabidhi vifaa vya shule
kwa wanafunzi waishio katika mazingira magumu vilivyotolewa na Chama cha
walimu (CWT)
Maadhimisho hayo yenye
kauli mbiu ya "Badili Fikra Kufikia Usawa wa Kijinsia kwa Maendeleo
Endelevu" yamekwenda sambamba na upimaji wa afya kwa magonjwa
yanayoambukizwa na yasiyoambukizwa bure, burudani mbalimbali, mashindano ya mchezo
wa mpira wa miguu kwa wananwake na mpira
wa pete.