Moja ya mradi uliozinduliwa na mbio za mwenge wa uhuru tarehe 14.05.2017 na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017, ndugu Amour Hamad Amour |
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka
2017 ndugu Amour Hamad Amour amewapongeza
viongozi na wananchi wa halmashauri ya wilaya ya masasi kwa kuanzisha na
kusimmaia miradi mizuri na yenye tija
kwa wananchi kama serikali ya awamu ya
tano inayosisitiza juu ya uanzishaji wa
miradi ambayo inalenga kutoa huduma kwa wananchi ikiwemo elimu,afya na miradi
ya kukuza uchumi .
Amour alitoa pongezi hizo wakati wa kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi
kwenye miradi mitano yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni mbili wakati wa
mbio za mwenge wa uhuru wilayani humo tarehe 14.05.2017 kwa kushuhudia ubora wa miradi hiyo ambayo
inalenga kutatua kero kwa wananchi.
Amour aliwaeleza viongozi na wananchi kwa
ujumla kuwa serikali ya awamu ya tano inalenga kuboresha huduma mbalimbali kwa
wananchi ikiwemo afya, elimu na kukuza uchumi kwa kushiriki shughuli za uzalishaji
mali kupitia viwanda vidogovidogo na
vikundi wa ujasiliamali.
Amour
alifafanua kuwa utekelezaji mzuri wa
miradi ambayo inatatua moja kwa moja kero za wananchi itarahisisha wananchi
kuutekeleza ujumbe wa mwenge kwa mwaka 2017 usemao “shiriki katika uchumi wa viwanda
kwa maendeleo ya nchi yetu” maana kama watu watakuwa na uhakika wa
kupata huduma za afya, maji na kuwa na kuwezeshwa kukuza uchumi ni dhahiri kuwa
tutakuwa tumeitekeleza kwa vitendo dhana ya Tanzania ya viwanda.
Mwenge ukiwa wilayani masasi uliweza kupitia
miradi ya ujenzi wa wodi ya akina mama na watoto katika kituo cha afya cha
chiwale, ujenzi wa ofisi ya chama msingi cha chamali kilichopo lukuledi,mradi
wa maji wa mpindimbi, soko la kisasa la mazao ya bustani kata ya chiwata na
kugawa hundi kwa vikundi vya wanawake na vijana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi bibi Changwa Mkwazu akipokea Mwenge wa Uhuru tayari kwa ukimbiza katika eneo lake
No comments:
Post a Comment