Mgeni rasmi Bi.Eufrosina
Chikojo (Afisa Tawala (W) Masasi akiwahutubia wananchi (hawapo kwenye picha)
kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake
duniani 2017 yaliyofanyika kiwilaya katika kijiji cha Lukuludi B.
Bi.
Eufrosina Chikojo, Afisa Tawala(W) masasi akikagua vikundi vya ujasiriamali
kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika kijiji cha
Lukuledi B siku ya tarehe 08.03.2017
Bi.
Eufrosina Chikojo, Afisa Tawala(W) Masasi akikabidhi hundi za mikopo kwa vikundi vya wajasiliamali vilivyopo kata ya lukuledi
kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika kijiji cha
Lukuledi B siku ya tarehe 08.03.2017
Bi.
Eufrosina Chikojo, Afisa Tawala(W) Masasi akiendeea kukabidhi hundi za mikopo kwa vikundi vya wajasiliamali vilivyopo kata ya lukuledi
Katika kuelekea Tanzania ya
viwanda, ili wananwake wawe msingi wa mabadiliko kiuchumi inapaswa wajengewe
uwezo wa kitaaluma, kibiashara, upatikanaji wa masoko na mikopo ili waweze
kushiriki kwa usawa na kunufaika na fursa zilizopo badala ya kuwa wasindikizaj.
Hayo yalisemwa na mwakilisha
wa Mkuu wa Wilaya ya Masasi Bi. Eufrosina Chikojo wakati akiwahutubia wananchi
katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kiwilaya katika
Kata ya Lukuledi wilayani Masasi na kusisitiza kuwa ili wananwake waweze
kushiriki kwenye uchumi wa viwanda ni lazima wapewe elimu ya kutambua fursa
zilizopo na namna ya kuzitumia.
Chikojo alisema kuwa kauli mbiu
ya siku hii ya wananwake inayosema Tanzania
ya viwanda, wanawake ni msingi wa mabadiliko ya kiuchumi ”, itatekelezwa
kwa vitendo endapo mwananke atapata elimu ya kutosha itakayo mwezesha kutambua na kutumia fura za kibiashara katika
kukuza uchumi wa kaya na taifa kwa ujumla kwani wao ndio walezi wakuu wa
familia katik jamii zetu.
Hivyo, kutokana na
mabadiliko tunayoyaendea kuna haja ya wanaume na jamii kwa ujumla kuona umhimu wa kumkinga mtoto wa kike na madhara mabaya ikiwemo kutompeleka shule,
ndoa za utotoni na tatizo la mimba kwa kuwa ndiye mwenye nafasi kubwa katika
kulea familia na jamii kwa ujumla.
Katika kuwawezesha wanawake
Halmashauri inapaswa kutenga fedha asilimia tano (5%) ya mapato yake ndani ili
kuweza kuwakopesha kwa riba nafuu. Aliwatia moyo akina mama waliokopeshwa fedha
na Halmashauri kufanya marejesho kwa ufasaha ili wengine waweze kupata mikopo
hiyo.
Bi. Chikojo amekemea tabia
ya wanaume kuwabagua wanawake kwa kuwanyima haki yao ya msingi ya kumiliki
raslimali zikiwemo ardhi, nyumba, mifugo na fursa zingine za kiuchumi pamoja na
kutowashirikisha katika utoaji wa
maamuzi ndani ya familia iachwe kwani nchi yetu inapoelekea katika uchumi wa viwanda
wanaume wanapaswa kutoa fursa kwa wanawake kushiriki katika shughuli za
uzalishaji mali.
Katika maadhimisho hayo Bi Chikojo
alikabidhi hundi za jumla ya shilingi 125,500,000/= kwa vikundi 72 kati ya
fedha hizo shilingi 54,900,000/= zilizokabidhiwa kwa vikundi 27 vya wanawake na
jumla ya wanawake 587 watanufaika na mikopo hiyo.
wanavikundi wakionesha bidhaa mbele ya mgeni rasmi
|
No comments:
Post a Comment