Katibu tawala wa mkoa wa mtwara ndugu Alfred Luanda akifungua mafunzo ya utengenezaji
wa tovuti za serikali kwa Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma yaliyofanyika mtwara
kuanzia tarehe 20 hadi 27 machi, 2017
Uimarishaji wa mifumo ya sekta za umma kupitia mradi wa PS3 ikiwemo uanzishwaji na
uhuishwaji wa Tovuti katika taasisi za umma utasaidia serikali kuimarisha utoaji wa taarifa kwa umma
kwa haraka na kwa wakati hali itakayo boresha utawala bora katika kuwahudumia
wananchi kwa uwazi.
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara
ndugu Alfred Luanda wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya utengenezaji wa tovuti za
serikali kwa mikoa ya Lindi, Mtwara na
Ruvuma yaliyofanyika kwa muda wa siku nane kuanzia tarehe 20 hadi 27, Machi,
2017 na kueleza kuwa mafunzo hayo yatawajengea uwezo Maafisa Habari na TEHAMA
kuweza kuendesha tovuti za serikali vizuri katika kuwahabarisha wananchi.
Luanda amewaeleza washiriki kuwa uboreshaji
wa tovuti za serikali utawezesha wananchi kupata fursa na haki ya kupata habari
na taarifa kwa njia ya mtandao ambayo
ndio njia ya haraka zaidi.
“Mnapaswa kufahamu kuwa upatikanaji wa
taarifa kwa umma ni suala la kisheria, hivyo baada ya mafunzo haya mtakuwa
mmepata uwezo zaidi wa kuandaa na kutangaza taarifa na fursa mbalimbali za
uwekezaji zilizopo kwenye taasisi zenu”
alifafanua Luanda
Uimarishaji wa mifumo ya sekta za umma
unaofadhiliwa na shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) ulianza
mwaka 2016 na utadumu kwa miaka mitano (5) ambapo jumla ya Halmashauri 93
katika mikoa 13 ya Tanzania bara pamoja na serikali kuu zitanufaika.
No comments:
Post a Comment