Kaimu Mkuu wa Mkoa wa
Mtwara Mheshimiwa Evod
Mmanda (aliyevaa Tai) akitoa maelezo maafisa Habari na Tehama baada ya kuzindua Tovuti za serikali zilizotengenezwa kwa mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma katika ukumbi wa Tiffany Diamond Hotel machi 27, 2017 (wa kwanza kulia ni kiongozi wa wawezeshaji ndugu Edgar Mdemu
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara mheshimiwa Evod Mmanda (wa tatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wawezeshaji wa mafuno ya utengenezaji wa Tovuti za serikali
Kaimu Mkuu wa
Mkoa wa
Mtwara mheshimiwa Evod Mmanda (wa tatu kulia) akiwa kwenye picha ya
pamoja na baadhi ya maafisa Habari na Tehama waliowezeshwa kutengeneza tovuti za taasisi zao.
Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mheshimiwa Evod
Mmanda amewataka maafisa habari wa taasisi
za serikali kuhakikisha wanatumia tovuti za serikali zilizotengenezwa kutoa
taarifa sahihi na kwa wakati ili kuepusha changamoto ya upotoshaji taarifa
mbalimbali za serikali kwa umma.
Mmanda aliyasema hayo wakati wa kufunga
mafunzo ya siku saba ya uanzishaji wa Tovuti za serikali yaliyofanyika katika
ukumbi wa Tiffany Diamond Hotel na kueleza kuwa maafisa habari ndio wanawajibu
wa kutoa taarifa sahihi kwa umma, hivyo viongozi wa Taasisi za Serikali hawatakiwi
kuzuia taarifa muhimu kwa wananchi kuingizwa kwenye Tovuti ili kuimarisha
utawala bora unaozingatia uwazi na uwajibikaji kwa umma.
Mmanda aliongeza kuwa kupitia tovuti hizo
wananchi na wadau wataweza kupata fursa
ya kuandika au kutoa malalamiko yao moja kwa moja kwenye tovuti ya taasisi
husika na kupata majibu kwa wakati bila kusumbuka kwenda ofisi za Taasisi hiyo
hali ambayo itapunguza gharama na upotevu wa muda katika kupata huduma wanayotaka.
“Mnapaswa kufahamu kuwa upatikanaji wa
taarifa kwa umma ni suala la kisheria, hivyo uwekaji wa taarifa kwenye tovuti
za kutoa taarifa na kutangaza fursa mbalimbali
za uwekezaji zilizopo ni la lazima sio utashi wa mtu ni lazima taarifa
hizi zihuishwe kila mara ili ziendane na wakati” aliagiza Mmanda.
Aidha Mmanda alieleza kuwa Uwekaji wa taarifa
za taasisi kwenye tovuti unaweza kuwasaidia
wawekezaji kujua fursa zilizopo
katika taasisizetu kwani atakuwa na uwezo wa kufahamu awekeze kwenye nini na kwa kiasi gani ili awe kupata
faida.
Kwa
Upande wake Mkuu wa timu ya wawezeshaji, Edgar Mdemu amesema mradi huo
unaodhaminiwa na USAID umezindukiwa leo kitaifa mjini Dodoma na kwamba
wanatarajia matumizi ya Tovuti yatasaidia kuimarisha utawala bora na
ushirikishwaji wa raia katika
utekelezaji wa shughuli za serikali kwa uwazi.
Mafunzo
ya utengenezaji wa Tovuti yalifunguliwa Machi 20 na kufungwa Machi 27 ambapo
kitaifa zoezi la ufungaji limefanyika mjini Dodoma.Uimarishaji wa mifumo ya sekta za umma unaofadhiliwa na
shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) ulianza mwaka 2016 na
utadumu kwa miaka mitano (5) ambapo jumla ya Halmashauri 93 katika mikoa 13 ya
Tanzania bara pamoja na serikali kuu zitanufaika.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara mheshimiwa Evod Mmanda akiitoa hotua wakati ya kufunga mafunzo ya utengenezaji wa tovuti za serikali kwa mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma na kuzizindua rasmi. |
No comments:
Post a Comment